Sura 3

1 Wakumbushe kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila kazi njema. 2 Wakumbushe kutomtendea mtu yeyoteubayawaepuke majibizano,wawape nafasi watu wengine katika kufanya maamuzi na kuonyesha unyenyekevu kwa watu wote. 3 Kwa kuwa hapo awali sisi pia tulikuwa na mawazo potofu na wakaidiwaasi. Tulipotoshwa na kufanywa watumwa wa tamaa na anasa mbalimbali. 4 Lakini wakati ukarimu wa Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana, 5 haikuwa kwa matendo yetu ya haki tuliyoitenda, bali alituokoa kwa neema yake.alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu. 6 Mungu alimwaga Roho Mtakatifu kwa wingi juu yetu kupitia mwokozi wetu Yesu Kristo. 7 Alifanya hivi ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi wenye tumaini la uzima wa milele. 8 Huu ni ujumbe wa kuaminika. Ninataka myanene mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu wawe waangalifu katika kutenda mema. Mambo haya ni mazuri na yanafaa kwa kila mtu. 9 Lakini jiepusheni na mijadala ya na nasaba, mashindano na migongano kuhusu sheria. Mambo hayo hayana faida na hayafai. 10 Mkataeni yeyote anayesababisha migawanyiko kati yenuBaada ya onyo moja ama mawili, 11 jueni kwamba mtu wa jinsi hiyo ameiacha njia iliyo sahihi na anatenda dhambi na kujihukumu mwenyewe. 12 Nitakapomtuma kwako Artema au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi. 13 Fanya kila uwezalo kuwatuma Zena mwanasheria, na Apolo, pasipo kupungukiwa na kitu. 14 Watu wetu lazima wajifunze kujishughulisha katika kazi nzuri ambazo zinatimiza mahitaji muhimu ili kwamba wasije wakawa wasiozaa matunda. 15 Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimie wale wanaotupenda katika imani. Neema na iwe nanyi nyote.