Sura 1

1 Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli iletayo utauwa, 2 Wapo katika tumaini la uzima wa milele ambao Munguasiyeweza kusema uongo, aliuahidi tangu milelekabla ya enzi zote za wakati. 3 Kwa wakati uliofaa alilifunua neno lake katika ujumbe alionipa mimi kuhubirilinipasa kufanya hivi kwa amri ya Mungu mwokozi wetu. 4 Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani yetu tunayoshiriki sote. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu. 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili upate kupanga mambo ambayo bado hayajakamilika na kuweka wakfu wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasioshuhundiwa mabaya au wasiotii. 7 Ni muhimu kwa mwangalizi, kama msimamizi wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu mwenye kiburi, hakasiriki haraka, si mraibu wa mvinyo, si mgomvi na asiwe mwenye tamaa. 8 Badala yake: awe mtu mkarimu, apendaye wema, mwenye busara, mnyoofu, mtakatifu na anayejidhibiti. 9 Awezaye kushika sana ujumbe wa kuaminika uliofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya ukweli na kuwarekebisha wale wanaompinga. 10 Kwa kuwa kuna waasi wengi, wanenao matupu na wandanganyao, hasa wale wa tohara. Maneno yao ni ya upuuzi.Wanandanganya na kuwaongoza watu katika upotovu. 11 Ni lazima kuwazuiawatu kama haoWanafundisha yale wasiopaswa kwa faida za aibu na kuharibu familia zote. 12 Mmoja wa manabii wao amesema "Wakrete daima ni waongo, wanyama wabaya, walafi wavivu." 13 Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo warekebishe kwa nguvu,ili kwamba waweze kusema kweli katika imani, 14 Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli. 15 Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Bali kwa walioharibika na wasioamini, hakuna kilicho kisafi, lakini akili zao na dhamiri zao zimeharibika. 16 Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni machukizo, wasiotii, na wasiofaa kitu kwa kazi yo yote njema.