1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, 2 kwa watu watakatifu wa Mungu na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu. 3 Tunatoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na tunawaombea kila mara. 4 Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa watu wote watakatifu wa Mungu, 5 kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenuMlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika katika neno la ukweli, injili 6 ambayo imekuja kwenu. Na kwa njia hiyo hiyo, Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni koteImekuwa ikifanya hivi ndani yenu tangu siku mlipoisikia na kufahamu neema ya Mungu katika kweli. 7 Hii ndiyo injili kama mlivyojifunza kutoka kwa Epafra,mtumishi mwenzetuambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa ajili yetu. 8 Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho. 9 Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujakoma kuwaombea.Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho, 10 Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa bwana katika njia zipendezazo Bwana.Tumekua tukiomba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu. 11 Tunaomba muweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wakekatika uvumilivu na ustahimilivu wote. 12 Tunaomba kwamba kwa furahamtatoa shukrani kwa Baba aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru. 13 Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza, akatuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa. 14 Katika mwanae tuna ukombozi na msamaha wa dhambi. 15 Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana,mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote. 16 Kwa kuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. 17 Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. 18 Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo, na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote. 19 Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake, 20 na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Akapatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni. 21 Nanyi pia, kwa wakati mmoja, mlikuwa mmetengwa na Mungu na mlikua maadui katika akili na matendo maovu. 22 Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo.Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake, 23 kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hii ndiyo injili ambayo ilihubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi. 24 Sasa nayafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa. 25 Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulitimiza neno la Mungu. 26 Huu ni ukweli wa siri iliyofichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika yeye. 27 Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua ulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli miongoni mwa Mataifa,Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao. 28 Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtukwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo. 29 Kwa ajili hii, mimi najibiidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza.